top of page

Acheni Acheni

(Mwenyezi ameniumba, akanileta kati

yenu, niwakumbushe watu wake thamani

yenu duniani) x2 (Acheni acheni kufa

moyo, acheni acheni kukata tama.Yeye

aliyewaumba anaijua kazi yake) x2


Aliijua asili yenu hata kabla

hamjaumbwa, Ramani ya maisha yenu,

yote imo mikononi mwake, magonjwa

yanayowatesa na maumivu yasiyokoma,

ni mdogo kuliko yale aliyoyaponya mwenyewe


Hali mbaya ya kiuchumi, mlo mmoja madeni

mengi, ni njia ya kunyenyekea na kumpa

Mungu ukuu, misiba inayowaliza mnapofiwa

na ndugu zenu, ni njia ya wapendwa wenu

kwenda mbinguni wakafurahi


Maumivu ya kuonewa kudhulumiwa

kusingiziwa, ni nafasi ya kusamehe na

kuishi kwa utakatifu. Matatizo ya ndoa

zenu na migogoro ya familia, ni bahati

mmejaliwa ya kuishi kwa uvumilivu

Bebeni misalaba uyenu, nyamazeni

msinungunike huo ndio wokovu wenu

shikilieni msiachie

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page