Alfajiri ya Kupendeza
- J.C Shomally
- Oct 5, 2023
- 1 min read
Updated: Oct 6, 2023
Alfajiri ya kupendeza, ni siku njema siku yenye baraka, Jua limekwishachomoza, laamsha wote waliolala, Ndege nao wanalialia kumshukuru Muumba (njooni) (Njooni baba, mama na watoto njoni wote mbele za Bwana Tumtolee shukrani zetu, kwa kutoa sadaka) x2
Ndege wanamshukuru, kwa sauti za kupendeza Na sisi tumshukuru, kwa zawadi alizotupa (njooni)
Wanyama pia na mimea, vyote vimeumbwa na Mungu Vitu vyote vya duniani, vyapaswa kumshukuru Mungu (njooni)
Kaiumba dunia hii, kaweka giza pia mwanga Mchana tufanyeni kazi, usiku na tupumzike (njooni)

Comments