top of page

Ametamalaki

Updated: Jan 29, 2024


Ametamalaki, ametamalaki Bwana ametamalaki, mbinguni ni yeye, ametamalaki Bwana ametamalaki, duniani ni yeye, ametamalaki Bwana ametamalaki, ametamalaki, ametamalaki Bwana ametamalaki

  1. Njooni na vinanda ngoma zeze vinubi, tumpigie Mungu wetu mziki mtakatifu

  2. Malaika mbinguni wanamsifu Mungu, na duniani pia asifiwaye ni Mungu wa milele.

  3. Asubuhi mapema ndege hulia lia, wakisifu pia wakishukuru kwa sauti za shangwe.

  4. Tazama sura yako na ya jirani yako, muonekano huo ni mfano wake mwenyezi Mungu.

  5. Uhai wetu upo mikononi mwa Bwana, autoaye ndiye auchukuaye milele milele.

  6. Uwepo wake unaonekana wazi, kwa matendo ya huruma ayatendayo kila siku

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page