top of page

Amin Amini Nawaambia

Updated: Oct 19, 2023



  1. Amin, amin, nawaambia, ninawaambia Amin, amin, mmoja wenu, atanisaliti Nitampiga mchungaji wa kondoo oo Na kondoo wa kundi lake watatawanyika*2

  2. Mwana wa Adamu aenda zake, ilivyoandikwa Ole ni wake mtu yule, amsalitiye Ole wangu, ole wako, umsalitiye Bwana Ingekuwa heri kwetu tusingelizaliwa *2

  3. Twaeni mle mwili wangu, uwe ukumbusho Twaeni mnywe damu yangu, iwe ukumbusho Nitampiga mchungaji wa kondoo oo Na kondoo wa kundi lake watatawanyika*2

  4. Amini, amini na kutubu, enyi mataifa Amini, amini na kutubu, turudi kwa Bwana Ole wangu, ole wako, umsalitiye Bwana Ingekuwa heri kwetu tusingelizaliwa *2

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page