top of page

Uko Juu

Updated: Dec 23, 2023


  1. Hufanani nasi, unang'ara na tena una enzi, una utukufu, Umepita zote, sifa tunazokutolea sisi, nao malaika oooh!

  2. Walikuimbia, baba zetu lakini hazikwisha, sifa zako wewe, Na watakatifu, wanaimba na hazimaliziki, tenzi hazitoshi ooh!

  3. Mimea ya nchi, yaeleza inapopukutika, kuhifadhi maji, Kwamba wewe Bwana, hupungui unajua kuumba, hupitiwi neno ooh!

  4. Kinyonga mdogo, anageuka rangi kujilinda, bila ya bunduki, Anafafanua, umakini ndani ya kazi yako, isiyo dosari oho

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page