Beba Mikononi
- Alfred Osonga
- Oct 21, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 23, 2023
Tusimame ndugu twende kwake Bwana (kweli) Usisite ndugu amka twende hima
Peleka kwa moyo, moyo wa mapendo (kweli) Peleka kwa Bwana uliyojaliwa
Sadaka ya fedha, fedha za mifuko (ndugu) Amka upeleke mezani kwa Bwana
Mavuno mifugo, ni mali ya Bwana (kweli) Tupeleke kwake atazipokea
Mkate divai tupeleke kwake (leo) Tupate baraka mbele zake Bwana
Twende ndugu twende, mbele zake Bwana (twende) Tupeleke nafsi zetu kwake Bwana

Comments