Bwana Anakuja II
- Conrad Mghanga
- Oct 22, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 25, 2023
Bwana anakuja Bwana anakuja (Bwana) Bwana anakuja kwetu kutuokoa x2.
Tutayarishe mioyo, kwa ujio wake Bwana, ili tupate okoka, kwani yeye ndiye Kristu, Mwokozi wa ulimwengu, yeye atatuokoa.
Mizigo yote ya dhambi, na tuiweke pembeni, Bwana aingie kwetu, kwani yeye ndiye Kristu, Mwokozi wa ulimwengu, yeye atatuokoa.
Mliovunjika nyoyo, mkaribisheni sasa, mpate kufarijika, kwani yeye ndiye Kristu, Mwokozi wa ulimwengu, yeye atatuokoa.
Wagonjwa wote wa mwili, na wale pia wa roho, njooni kwake anaponya, kwani yeye ndiye Kristu, Mwokozi wa ulimwengu, yeye atatuokoa.

Comments