top of page

Bwana Unihifadhi Mimi

Updated: Apr 29, 2024

Bwana, unihifadhi mimi, Nakulilia wewe mchana kutwa


  1. Unisikilize, maana mimi ni fukara, ee Bwana.

  2. Wewe ni Mungu wangu, unionee huruma, ee Bwana.

  3. Mimi ninakulilia, mchana kutwa, ee Bwana.

  4. Wewe u mwema, na mwenye huruma, ee Bwana.

  5. Umejaa upendo, kwa wote wanaokuomba, ee Bwana.

  6. Usikie sala yangu, uangalie kilio changu, ee Bwana.

  7. Siku za tabu, nakuita, ee Bwana.

  8. Hakuna Mungu, aliyekama wewe, ee Bwana.

  9. Hakuna awezaye kufanya, unavyofanya wewe, ee Bwana.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page