Harusi Kidededede
- Alfred Osonga
- Oct 20, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 23, 2023
Bwana harusi na bibi harusi, leo mmefunga ndoa ya maisha, Kaeni kwa amani kidededede) x2
Jitulize mjisikie sukari, siku ya leo ni yenu, Furahini, mmepambwa maua mnapendeza
Bwana arusi kwanza wachangamka, bibi arusi chachawa, Chezacheza, penzi lenu leo limekamilika
Mapenzi yenu yote yatasitawi, hakika yatasitawi, Yatamea, kama ule mwerezi wa Lebanoni
Baraka zake Mungu ziwashukie, kaeni pasipo shida, Siku zote nyumba yenu iwe hekalu la Mungu.

Comments