top of page

Hila Zimevunjwa

  1. Mungu alipopanga ukombozi kusudi kutuosha dhambi hizi akakubali kwamba ye mwenyezi afe kifo kibaya kionezi mti wakamuwamba kama mwizi wakidhani ya kwamba ameshindwa amefufuka Bwana na mwokozi kazivunja hila Lusiferi katukomboa wana wa Mwenyezi twaimba ndiyo maana nyimbo nzuri Amefufuka Bwana na mwokozi kazivunja hila za Luciferi, katukomboa wana wa Mwenyezi twaimba ndiyo maana nyimbo nzuri

  2. Mungu akakubali kuonewa hakuweka wakili kutetewa nguo bila hiari kavuliwa kapigwa misumari kazomewa akakubali kusali kuombea wauaji wapate msamaha

  3. Mungu atufundisha kujitoa ya wengi maisha kuokoa na anatukumbusha kupokea yanayotutisha kumwendea tusije kukatisha njema nia ili kuyapisha ya dunia

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page