top of page

Hosanna Mwana wa Daudi

Updated: Nov 18, 2023

Hosanna Mwana wa Daudi, ndiye mbarikiwa Yeye ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli Hosanna juu Mbinguni enyi watu wote pigeni makofi Mshangilieni Mungu kwa shangwe kubwa


Kwa sababu Bwana aliye juu ni mwenye kutisha Ndiye mfalme mkuu wa dunia yote


Atawatisha watu wa dunia chini yetu na mataifa chini ya miguu yetu


Atatuchagulia urithi wetu fahari ya Yakobo ambaye alimpenda


Mwimbieni Mungu imbeni, mwimbieni mfalme wetu mwimbieni


Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote imbeni kwa akili


Mungu awamiliki mataifa Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu


wakuu wa dunia wamekusanyika wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu


Maana ngao za dunia zina Mungu ametukuka sana

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page