Hossanna Mfalme wa Israeli
- Conrad Mghanga
- Oct 22, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 25, 2023
Wakatwaa matawi matawi ya mitende wakatoka nje ili kwenda kumlaki, wakipiga kelele hosana hosana mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana
Yesu alikuwa amepanda mwanapunda kama vile maandiko yanavyosema, usiogope ee binti Sayuni tazama mfalme wako anakuja kapanda punda
Mambo hayo yalikuwa mageni kwa wote hata wanafunzi wake hawakufahamu, lakini Yesu alipokwisha kutukuzwa ndipo walipokumbuka ilivyoandikwa
Ishara aliyokuwa ameifanya huko Bethania ilikua ya ajabu, ya kumfufua Lazaro aliyekufa hivyo wengi walitoka ili wamuone

Comments