top of page

Ingawa Hakutenda Jeuri

Ingawa hakutenda jeuri kinywani mwake hapakuwa na hila, lakini Bwana aliridhika kumchukua amemhuzunisha x2

  1. Kama mzizi katika nchi kavu, yeye hakuwa na umbo na uzuri, alitengwa na alidharauliwa, mtu aliyejaa huzuni nyingi.

  2. Amechukua masikitiko yetu, amejitwika pia huzuni yetu,tulimdhania amepigwa na Mungu, alijeruhiwa kwa makosa yetu.

  3. Alichubuliwa kwa maovu yetu kwa kupigwa kwake sisi tumepona,sote kama kondoo tumepotea, kila mmoja ameshika njia yake.

  4. Kwa kuonewa pia kuhukumiwa,aliondolewa aliondolewa,na maisha yake maisha yake, ni nani atakayeisimuliwa.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page