top of page

Kama Yule Mmoja

Updated: Oct 28, 2023



1. Kama yule mmoja kati ya wale kumi aliyerudi kusema sante.

Ndio maana leo na mimi nimerudi, kumwambia Baba asante nashukuru.


Kama mmoja kati ya wale kumi nami nimerudi kusema asante x2

Asante nashukuru mbelezo ninarudi nakuja na zawadi uipokee ijapo ni kidogo kulingana namema uliyonitendea Baba pokea.


2. Tunaleta Baba mazao ya mashamba kazi ya mikono yetu wanadamu Tunaleta fedha za mifukoni mwetu malipo ya kazi zetu wanadamu.


3. Mkate divai tunavyolutolea vigeuze mwili na damu ya Mwanao Ee Baba sikia sala zetu leo na utujalie ondoleo la dhambi.


4. Ee Baba twaleta maisha yetu kwako kama shukrani kwa mengi ulo tenda Vyote tulonavyo Baba ni mali yako na sisi tu kazi yako ya mikono yetu


Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page