top of page

Karibu Moyoni Mwangu

Updated: Dec 25, 2023


Karibu moyoni mwangu leo Yesu wangu mpenzi, ukae na mimi siku zote za maisha yangu x2

  1. Nikitazama pande zote pande za dunia, nawaona watu wamejaa furaha moyoni na nyuso zao zimejaa furaha kamili, kwasababu Bwana, amewapa, furaha kamili.

  2. Nami Bwana ninatamani furaha ya kweli, niungane leo, na wenzangu, nikufurahie ni upokee Mwili Wako pia Damu Yako, nisione njaa, wala kiu, siku zangu zote.

  3. Ninakuja sasa ee Bwana kwa furaha kubwa, nipokee Bwana, Yesu wangu, nifurahi nawe mzigo mzito wa dhambi siutaki tena, ninakukabidhi, moyo wangu, pia mwili wangu.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page