top of page

Kina Hiki

Kina hiki kina maji mengi pande nne zimejaa, ee Bwana, Dunia nayo mji mkavu, wamemezwa watu wengi ee Bwana (Ona) watu wauana ovyo,(ona) vita navyo imezidi (Tena) magonjwa ya kushangaza Sasa Bwana tufanyeje sisi? (Tunalia tunalia Bwana twalilia ulimwengu huu Na machozi yetu sisi Bwana yakiokoe kizazi hiki Usimame tutetee Bwana tusaidie wanao) x2

  1. Maji yamekuwa mengi sana nashindwa kuvumilia, Sina msaada mimi Bwana naomba nihurumie

  2. Shida nyingi sana mimi Bwana zinazidi kunisonga, Nashindwa kuvumilia mimi ee Mungu nihurumie

  3. Dunia nayo yahuzunisha maovu yametawala, Watu nao wateseka sana ee Mungu tusaidie

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page