Kisha Nikaona
- Alfred Osonga
- Oct 15, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 23, 2023
Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya (Nikauona mji (mji ule), ule mtakatifu Jerusalem mpya ukishuka toka mbinguni) x2
Kwa maana mbingu ya kwanza na nchi ya kwanza, Zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena
Nikasikia sauti kubwa ikitoka, Kwenye kiti cha enzi, tazama maskani yake Mungu
Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, Naye atayafuta, machozi katika macho yao
Mauti maombolezo kilio maumivu, Hayatakuwapo, tazama yote yamekuwa mapya

Comments