top of page

Kristu Ametii kwa Ajili Yetu

Kristu ametii kwa ajili yetu hata kufa, kufa msalabani

1. Muwe na msimamo ule ule / aliokuwa nao Kristu Yesu.

2. Yeye kwa asili / alikuwa daima Mungu.

3. Yeye hakutaka kutumia usawa wake na Mungu / kwa kujifaidia mwenyewe.

4. Bali kwa hiari yake / aliachilia hayo yote.

5. Yeye akajitwalia/ hali ya mtumishi.

6. Akawa sawa na wanadamu / akaonekana kama mwanadamu.

7. Alijinyenyekeza na kutii mpaka kufa / hata kufa msalabani.

8. Kwa sababu hiyo / Mungu alimkweza juu kabisa.

9. Mungu alimpa jina lililo kuu zaidi / kuliko majina yote.

10. Ili kwa jina la Yesu / viumbe vyote vipige magoti.

11. Kila mtu akiri / ya kuwa Yesu Kristu ni Bwana.

12. Yeye ndiye Bwana / kwa utukufu wa Mungu Baba.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page