Mama Akaitika
- Benard Mukasa
- Oct 14, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 23, 2023
Hatari ikaja nikageuka mbio kumlilia - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee, Akaifungua mikono yake myema kanidaka - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee Nikalaza kichwa kifuani kwa mama nikihema- Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee
Wenye nguvu zao walibeba silaha, kupigana - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee, Wakapigania ndani ya nyumba yetu, hatari kuu - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee, Wakazidiana paa wakalipua,tumekwisha - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee
Kwenye familia migogoro ya ndoa shida tupu - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee, Watoto wakawa na maadili duni, balaa tu - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee, Na magonjwa lundo uchumi hohehahe, taabu tu - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee
Bibi yangu Eva alizaa laana duniani - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee, Mama yangu mwema akazaa wokovu,wa milele - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee, Nkakabidhiwa niwe mwanaye naye, mamangu ee - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee
Uovu wa watu ulishika hatamu kila kona - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee, Amani ikawa ndoto ya jua kali haipo ee - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee Hofu na mashaka vikafunika nchi,hatari kuu - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee
Baba wa kanisa akaniita shime tujiunge- Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee, Tusali rozari tumlilie mama wa amani - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee Atatusikia ataushusha mkono wa Yesu - Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee

Comments