Mama Maria Tunakusalimu
- Anonymous
- Nov 1, 2023
- 1 min read
Mama Maria Mama tunakusalimu, wewe uliyetukuka uwinguni x2
Tunajinyenyekeza mbele ya uso wako, tunakuimbia nyimbo zetu tunakusifu x 2
Ee Mama wetu utusikilize sisi wanao tunakusalimu.
Usitutupe tunapokujia, ee Mama wetu utukaribishe.
Tunakujia tukiwa na shida utupokee ee Mama wa Mungu.
Utupokee katika maovu, utuongoze katika maisha.

Comments