Mbali Kule Nasikia
- Hymns
- Nov 1, 2023
- 1 min read
Updated: Dec 25, 2023
Mbali kule nasikia malaika wa mbinguni wakiimba wengi pia wimbo huo juu angani:
Wachunga tuambieni sababu ya nyimbo hizo: mwenye kuimbiwa ni nani, juu ya nani sifa hizo.
Je hamjui jambo kuu la kuzaliwa Mwokozi? Habari ya wimbo huu ndiyo kumshukuru Mwenyezi.
Kweli, nasi twende hima tufike kule aliko, tuone mtoto na mama, tuwasalimie huko.

Comments