top of page

Mchungaji Mpenzi

  • Hymns
  • Nov 6, 2023
  • 1 min read

Mchungaji mpenzi hukuita uje

Katika zizi lake panapo salama;

Akina wanawake, waume vijana,

Yesu aliye kweli, huwaita kwake.


Huita kwa moyo wa huruma, ‘Uliyepotea uje kwangu‘

Hivi kukungoja anadumu, Bwana Yesu Mchunga.


Akatoa maisha kwa ajili yetu;

Ataka wapotevu waje kwake sasa;

Tusijihatirishe; Kwake tu salama;

Sikia wito wake, Mchungaji wetu.


Tusikawie tena, adui Shetani,

Kama mbwa wa mwitu, atatuharibu;

Tunaitwa na Yesu, Mkombozi wetu,

Tuingie zizini, panapo nafasi.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page