top of page

Meza Ipo Tayari

Updated: Dec 25, 2023


Meza yake Bwana ipo tayari, amekwisha andaa Bwana wetu Yesu, twende tukale chakula cha uzima x2

  1. Duniani hapa sisi tu wasafiri twaelekea kwake Mungu wetu, safarini twahitaji chakula hiki ili tupate nguvu za kutosha

  2. Tunapata neema tunaposhiriki meza yake Bwana kikamilifu, tujitayarishe basi tukampokee Bwana Yesu Kristu kwenye Ekaristi

  3. Mwili wake sio kama ile mana waliokula baba zetu jangwani, tule mwili na tunywe damu yake Yesu ili tupate uzima wa milele

  4. Tufungue mioyo tumkaribishe ili aingie ndani yetu, tutapata amani pia na furaha tukiwa naye Yesu kila wakati

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page