top of page

Millenium Mass

Updated: Dec 19, 2023



Bwana Bwana Bwana utuhurumie x4

Kristu Kristu Kristu utuhurumie x4

Bwana


UTUKUFU

Tunakusifu, tunakuheshimu, tunakuabudu, tunakutukuza

  1. Utukufu kwa Mungu juu mbinguni na amani kote ulimwenguni kwa watu aliowaridhia

  2. Twakushukuru Mungu kwa ajili ya utukufu wako mkuu Bwana ni wewe Mungu mfalme wa mbinguni

  3. Baba Mwenyezi Bwana Yesu Kristu Ee Mwana wa pekee Yesu Kristu Ee Mungu Bwana wako Baba

  4. Uondoaye dhambi za ulimwengu Utuhurumie tuhurumie maombi yetu Baba upokee

  5. Uketiye kuume kwake Baba utuhurumie tuhurumie kwa kuwa ndiwe pekee mtakatifu

  6. Pekee yako peke mkuu Ewe Yesu Kristu pamoja nawe Roho mtakatifu milele yote


NASADIKI

1. Ladies: Nasadiki kwa Mungu mmoja - Nasadiki

Men: Ndiye Baba yetu Mwenyezi -

Ladies: Muumba mbingu pia dunia -

Men: Nasadki kwa Yesu Kristu -


(Kweli) Nasadiki, nasadiki, ninasadiki x2


2. Mwana wa pekee wa Mungu -

Aliyezaliwa kwa Baba -

Akapata mwili kwa roho -

Kazaliwa naye Bikira -


3. Kisha yeye kasulubiwa -

Kwa amri yake Pilato -

Kwa ajili yetu kateswa -

Akafa na akazikwa -


4. Kafufuka katika wafu -

Akapaa juu mbinguni -

Ameketi kuume kwake -

Baba yetu Mungu Mwenyezi -


5. Ndipo atakapotokea -

Kuhukumu wazima na wafu -

Kwake Roho Mtakatifu -

Kwa kanisa la Katoliki -


6. Ushirika wa watakatifu -

Ondoleo la dhambi zetu -

Nangojea 'fufuko wa mwili -

Na uzima wa milele -

BABA YETU

1. Baba yetu uliye mbinguni - jina lako litukuzwe

Ufalme wako utufike - utakalo lifanyike x2

Duniani kama mbinguni - jina lako litukuzwe


2. Tupe leo mkate wetu -

Mkate wetu wa kila siku -

Tusamehe makosa yetu -


3. Kama vile twawasamehe -

Wale waliotukosea -

Situtie kishawishini -


4. Walakini utuopoe -

Maovuni utuopoe -

Kwa kuwa ufalme ni wako -


5. Nguvu na utukufu pia -

Utukufu hata milele -

 
 
 

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page