top of page

Moyo wa Yesu

  1. Ee yesu utupee moyo wako wa mapendo wewe ndiwe kimbilio letu maishani kunakutumainia bwana siku zote tujawe moyo wa mapendo yako Ili tupate pumziko salama siku zote za maisha yetu


Moyo Mtakatifu wa yesu ni moyo wa mapendo

Moyo Mtakatifu wa yesu ni moyo wa huruma

Moyo Mtakatifu wa yesu ni moyo wa Amani

Moyo Mtakatifu wa yesu ni moyo wa faraja

Moyo Mtakatifu wa yesu twakutumainia wewe


2. Moyo wako ulipendwa huzuni na uchungu Kwa mapendo kwako kwa Kwetu Sisi wanadamu upendo kwa sasa uko wapi kati yetu ee Yesu twaomba huruma yako tujalie neema zako maishani

Tuishi ndani ya pendo lako


3. Haki za wengi walo wanyonge sinazimwa wanakosa wakimbilie wapi maishani tunajua moyo wako Yesu wa huruma Waite waje wafarijike tunajua wewe ni mungu wa wanyonge Waite waje wafarijike

HITIMISHO

Tujaze mapendo twakutumainia wewe bwana Katika safari twakutumainia bwana tujaze huruma twakutumainia wewe bwana Nitie faraja twakutumainia bwana Wewe ndiwe njia twakutumainia wewe bwana Nishike mkono twakutumainia bwana tufike salama twakutumainia wewe bwana Mbinguni uliko twakutumainia bwana

 
 
 

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page