Moyo Wangu
- Steve Limila
- Nov 3, 2023
- 1 min read
Moyo wangu tayari imezimika, siku zangu zimekoma, na kaburi tayari kunipokea njoo Bwana uniokoe
Sasa nakuita Bwana, njoo hima hima kwangu, jicho langu linakutazama Bwana wangu (Bwana wangu) Njoo uniondolee shida na mateso haya, moyo wangu unakutazama Bwana wewe ni ngao yangu
Na amini wewe Bwana niwe uwezaye kuni ondolea haya maumivu ya moyo wangu. Nakuomba wewe Bwana tazama mateso yangu usiutazame udhaifu wa moyo wangu.
Bwana wangu fungua sikio lako, sikio oh ho, fumbua macho yako oh, utazame wewe Bwana, niongoze Bwana wangu, mbinguni ah eh, niishi na wewe Bwana, wewe Bwana mbinguni milele yote. x2
Sikio usikie sauti yangu, macho yako utazame kilio changu, niongoze mbinguni kwa Mungu Baba, niishi na Bwana wangu milele yote, x2
Kila siku ninasongwa na Maneno ya ghihaka Bwana wangu, ndugu zangu wote wamenikimbia, njoo Bwana uniokoe.
Tazama na ibilisi anavyonisonga ili nijitenge nawe kamwe siwezi kabisa (Bwana wangu) Katika mateso haya na katika dhiki hizi, nitakuwa nawe Bwana wangu Mwokozi wa moyo wangu.
Ulikufa pale msalabani kwa ajili yangu, ninakushukuru kwa kunionyesha pendo lako la ajabu.

Comments