top of page

Mpendaneni Daima

Updated: Dec 23, 2023


  1. Mungu akaona si vyema mtu huyu awe peke yake Nitamfanyia mwenzake yule wanafanana naye Akaumba mwanamke, kamleta kwake mwanamume waishi pamoja

  2. Mungu akawapa uwezo watawale viumbe vyote Mungu akasema zaeni muijaze dunia kwa watu Baraka za Mungu Baba, zimewashukia tangu leo zaeni matunda

  3. Ewe mwanamume mpende mke wako kwa moyo wote Nawe mwanamke heshimu mume wako mtii daima, Ndoa ni maagano, kati ya watu wawili wapendanao

  4. Nyumba yenu iwe hekalu lake Mungu kanisa ndogo Nyumba ya amani upole na furaha nyumba ya sala Mungu ameunganisha mwanadamu asitenganishe daima dawamu

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page