top of page

Mpeni Kaisari

Updated: Nov 23, 2023


Vipaji tumepewa, mapato tumepata Lakini binadamu tunashindwa kushukuru Wakati tunaomba, tunajinyenyekesha lakini tukipata mikono yetu birika

Mpeni kaisari, yaliyo yake Mpeni Mungu (yale) yaliyo yake Mungu x2


Mifugo tunafuga, nafaka tunavuna Lakini kila siku tunakula na kusaza Kumbuka kuna wale, wasio na chochote hawawezi kupata, hata kikombe cha chai


Tunapofanya kazi, twapata mishahara Shughuli zetu sisi kuingia kwenye baa Ikiwa zitabaki, twakuja kanisani Twamtolea Mungu, shilingi moja na tano


Tukiwa na wagonjwa hatuwasaidii Wakati wamekufa tunachanga kwa huzuni twachukua mikopo, kwa mambo ya anasa Ujenzi wa kanisa, twalazimishwa kutoa.


Kumbuka Ibrahimu, alitoa mwanawe Kama sadaka kwake Mungu Baba wa mbinguni na Sisi kwa furaha, tupeleke zawadi itakayopendeza, kama ile ya Abeli

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page