top of page

Mpigieni Mungu vigelegele

Updated: Jan 13, 2024

Mpigieni Mungu vigelegele, mshukuruni Bwana kwa mema yote x2

Sop: Msifuni kwa nyimbo zenye kupendeza, mwimbieni mtukuzeni milele x2

Alto: Msifuni Mungu wenu, mshangilieni, mwimbieni mtukuzeni milele x2

Tenor: Mtukuzeni, kwa nyimbo nzuri za shangwe, mwimbieni mtukuzeni milele x2

Bass: Msifuni kwa matendo yake makuu, mwimbieni mtukuzeni milele x2

  1. Aliumba vitu vyote duniani, akatukabidhi sisi wanadamu Ni vyema tumshukuru Mungu wetu x2

  2. Jua lachomoza kwa wakati wake, tunapata mwanga na joto mwilini Ni vyema tumshukuru Mungu wetu x2

  3. Alipanga vyema majira ya mwaka, mvua hunyesha kwa wakati wake. (Ni vyema tumshukuru Mungu wetu x2)

  4. Pepo zavuma kusini kaskazini, zavuma mashariki na magharibi (Ni vyema tumshukuru Mungu wetu x2)

  5. Alipanga vilima na milima akapisha mito kwenye mabonde (Ni vyema tumshukuru Mungu wetu x2)

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page