Mungu Wangu Mbona Umeniacha
- Anonymous
- Oct 15, 2023
- 1 min read
Updated: Oct 22, 2023
Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha
Wote wanionao huncheka sana, Hunifyonya watikisa vichwa vyao husema hutegemea Bwana na amponye, Na amwokoe sasa maana apendezwa na yeye
Kwa maana mbwa wamenizunguka, Kusanyiko la waovu wamenisonga Yamenizua mikono na miguu, Naweza kuihesabu mifupa
Wanagawanya nguo zangu, Na vazi wanalipigia kura Nawe usiwe mbali, Ee Mungu wangu fanya haraka kunisaidia
Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu, Katikati ya kusanyiko nitakusifu Ninyi mnaomcha Bwana, msifuni, Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo mtukuzeni.

Comments