top of page

Mwamba wenye Imara

  1. Mwamba wenye imara, kwako nitajificha Maji hayo na damu, yaliyo toka humu Hunisafi na dhambi, hunifanya mshindi

  2. Kwa kazi zote pia, sitimizi sheria Nijapofanya bidii, nikilia na kuudhi Hayaishi makosa, niwe wa kuokoa

  3. Sina cha mkononi, naja msalabani Nilitupu, nifike, ni mnyonge, nishike Nilimchafu naja, nioshe nisijafa

  4. Nikungojapo chini, na kwenda kaburini, Nipaapo mbinguni, na kukwona enzini Roho yangu naiwe, rahani mwako wewe

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page