top of page

Mwokozi amezaliwa

Amka kinanda ngoma na zeze, zeze tulipige Ngoma na tucheze, Mwokozi amezaliwa x2 Mji wote ni furaha chereko na vifijo, Nao malaika wanaimba kwa furaha Gloria Gloria Gloria Gloria Gloria glo-ria


Bwana Yesu Kristu kazaliwa leo Bethlehemu Nao malaika wanashangilia Mbinguni


Waumini wote njoni kwa furaha tuimbe Chereko chereko kazaliwa Bwana aleluya


Tufurahi sote Bwana Yesu Kristu kazaliwa Amka kinanda ngoma pia zeze shangilia

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page