top of page

Mwokozi Wangu Yesu

Updated: Dec 21, 2023

Mwokozi wangu Yesu Hakika unanipenda, umenilisha mwili na damu umeninywesha (Yesu), (Yesu asante sana nakushukuru) x 2

  1. Bwana wangu Yesu hakika ninakupenda sana, Moyo wangu mimi ninakutolea

  2. Wewe Yesu, (Umenikaribisha mimi katika karamuyo, karamu ya chakula kilichoshuka toka mbinguni)

  3. Mwili wake Yesu chakula cha roho zetu sisi, damu yake Yesu kinywaji cha roho zetu sisi, (Wana heri wale wote wa naokula mwili wake, na kuinywa damu yake maana wataishi na Yesu)

  4. Umenipa mwili na damu yako umeninywesha,Umenishibisha na pia umeniburudisha, (Umeniimarisha najua sitapata njaa, hata kiu sitapata nikiwa na wewe Yesu wangu)

  5. Mwamba wangu mimi ni wewe Yesu Mwokozi wangu, Nguvu zangu mimi ni wewe Yesu Mwokozi wangu, (Nakutegemea Yesu najua sitaaibika na matumaini yangu yafike mbinguni kwako wewe

  6. Bwana wangu Yesu hakika ninakupenda sana, moyo wangu mimi ninakutolea wewe Yesu, (umenikaribisha mimi katika karamuyo, karamu ya chakula kilichoshuka toka mbinguni

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page