top of page

Nainua Moyo Wangu

1. Nainua moyo wangu, kwako wewe, ee Baba;

Unikinge na uovu, tumaini wewe tu.

2. Nijulishe njia zako, ‘nifundishe ukweli;

Hekimayo niongoze, tumaini wewe tu.

3. Ewe Baba, ukumbuke, wema wako milele;

Nifutie dhambi zangu, tumaini wewe tu.

4. Nitazame kwa huruma, ewe Mungu amini;

Nitubishe, mwenye dhambi, tumaini wewe tu.

5. Shida zangu angalia, ‘niokoe dhikini;

Nisamehe dhambi zangu, tumaini wewe tu.

6. Njia zake zote, Bwana, ni fadhili na kweli;

Niongoze, mtoto wako, tumaini wewe tu.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page