top of page

Nakula Mwili wa Yesu

Updated: Dec 23, 2023

  1. Nakula mwili wa Yesu, nakunywa damu ya Yesu Naburudika daima, narukaruka na Yesu naimba wimbo wa Yesu, nachezacheza na Yesu natembea naye Yesu, naenda kwetu Mbinguni

  2. Mwalimu wangu ni Yesu, tabibu wangu ni Yesu Mlinzi wangu ni Yesu, mimi nina usalama uhai wangu ni Yesu, mapito yangu ni Yesu, naenda na Bwana Yesu, naelekea Mbinguni

  3. Rafiki wangu ni Yesu, jabali wangu ni Yesu mshindi wangu ni Yesu, mimi nitashinda vita.Mpaji wangu ni Yesu , mlishi wangu ni Yesu mjali wangu ni Yesu, sina budi kumsifu

  4. Kaeni ndani ya Yesu, kaeni pamoja naye, na Yesu akae kwenu, mtashinda majaribu shikeni maneno yake, jifunzeni kwake Yesu, Yesu atawachukua, awapeleke Mbinguni

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page