Nakupenda Maria
- P.F Mwarabu
- Oct 22, 2023
- 1 min read
Nakupenda Maria Mama uliye bora , Furaha yangu Maria nikae nawe daima, Nipate neema zako nifike juu mbinguni) x2
Mama mwema Mariaunikinge unilinde , Nifanye yote mema nayo mabaya niyashinde
Uliye barikiwa Maria mpendelevu , Unijaze Baraka ili niwe mnyenyekevu.
Uyatulize Mama mashaka ya moyo wangu Neema za mwana wako zifariji roho yangu

Comments