top of page

Naondoka Mimi

Updated: Dec 23, 2023


  1. Naondoka mimi naenda kwa Baba, Nipeleke hiki nilichokipata, Japo kidogo, sitaona haya, Nimeamua, sitarudi nyuma

  2. Natembea mimi mwendo wa madaha, Nakanyaga chini kwa maringo tele, Naelekea altare ya Bwana, Nimkabidhi nilichojaliwa.

  3. Nimechangamka ninashangilia, Napiga kelele, kelele za shangwe Nachezacheza, najongea kwako, Ee Mungu Baba Nipokee mimi.

  4. Nafsi yangu mimi naileta kwako, Mkate divai, pia ninaleta Uigeuze mwili na damuyo, Chakula chetu, tunaosafiri

  5. Mavuno shambani mimi nimevuna, Mifukoni fedha nimekabidhiwa, Mimi ni nani, nisikushukuru, Baba nasema asante kwa yote.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page