top of page

Nena Nami Bwana

Updated: Dec 25, 2023

(Nena) nena nena nami Bwana, nena nena nena moyoni mwangu, kwa sauti ya upole nieleze akili zangu Bwana zikuelewe x2

  1. Neno lako ee Bwana ndiyo taa kuniongoza, pia tena ni mwanga katika njia zangu.

  2. Nimekusudia kwa moyo wote akili zote na nguvu zote, kuyafuata mafundisho mafundisho yako daima.

  3. Nipe neema ee Mungu wangu nisiwe shamba lenye mawe, nikusikie kwa saburi nitunze neno lako daima.

  4. Mimi hapa najitota kueneza neno lako, kwa watoto kwa vijana na wazee wakaokoke.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page