top of page

Neno Asante

Updated: Dec 19, 2023



Moyoni mwangu moyoni mwangu nisiposema neno asante nisipokiri wema wa Mungu, ulimi wangu ugandamane na kaakaa na kinywa changu mimi x2


  1. Ninakushuru Baba Mungu wangu kwa mema unayo nitendea Baba, siku zote ninawaza jinsi gani nitalipa nini mimi kwa shukrani

  2. Yote uliyoyatenda juu yangu nashindwa kusimulia Baba yangu, machozi yenye upendo na furaha yamelipamba shavu langu

  3. Leo ninaimba nyimbo za furaha ninageuka kushoto na kulia, nimeamsha vinanda na vinubi asubuhi na mapema ninaimba

  4. Umenishibisha mema ya mbinguni, pendo lako limetua ndani yangu, Furaha imetawala moyo wangu jinsi ninavyokusifu Mungu wangu

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page