top of page

Nikupe Nini Wewe, Bwana

Updated: Dec 19, 2023



(Nikupe nini wewe, Bwana Mungu wangu) x2.

(Kwa mema mengi ee Bwana, unayonitendea mimi maishani Mwangu) x2


  1. Umenilinda wiki nzima - Baba nashukuru, Afya ya mwili na ya roho - Baba umenipa

  2. Umenijalia watoto - Baba nashukuru, Kazi na mali umenipa - Baba nashukuru

  3. Pumzi ya bure umenipa - Baba nashukuru, Kwa vita njaa na magonjwa - Umeniwezesha.

  4. Nikiwa safarini Bwana - Unaniongoza, Waniepusha na ajali - Baba nashukuru.

  5. Akili pia na imani - Umenizidishia, Sauti nzuri umenipa - Nikuimbie wewe.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page