top of page

Nimempokea Yesu

Updated: Dec 23, 2023


  1. Nimempokea Yesu mzima kwenye Ekaristi Nguvu zake za mbinguni na baraka amenipa Sasa moyo wangu mimi unafurahi Roho yangu mimi inashangilia (kweli)

  2. Nimempokea Yesu mzima kwenye maandiko Bibilia takatifu kweli nimeisoma mafundisho yake yote yamenigusa Nikaamua nijikabidhi kwake (kweli)

  3. Nimempokea Yesu mzima kwenye mahubiri Mahubiri yake yamejaa hekima na busara maneno ya kinywa chake ni taa yangu Mwanga wa kuniongoza nipitapo (kweli)

  4. Nimempokea Yesu mzima kwenye jumuiya Majirani marafiki ndugu zangu na jamaa nyote mnaonijua nawaambia Mimi si wenu, mimi ni wake Yesu (kweli)

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page