top of page

Nimeonja Pendo Lako

Updated: Dec 23, 2023


  1. Nimeonja pendo lako nimejua umwema, Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe nitawaongoza vyema waimbe kwa furaha Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe

  2. Kina mama simameni piga vigelegele - Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe, na kina Baba nyanyukeni, mkapige makofi - Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe

  3. Watu wote lesa lesa chezeni kwa furaha - Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe, Inua mikono juu, mshangilieni Bwana - Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe

  4. Watawa washangilie makasisi waimbe - Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe, Walei waruke ruke waseme aleluya nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe

  5. Vitambaa mikononi vipeperushwe juu, Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe na vichwa viyumbeyumbe kwa mwendo wa maringo – Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe

  6. Nitakushukuru mimi na nyumba yangu yote – Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe nitayatangaza haya maisha yangu yote – Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page