top of page

Nina Yesu Moyoni wangu

Updated: Dec 23, 2023


Nina Yesu moyoni mwangu, mimi nina Yesu moyoni mwangu; Nimeupata ukombozi nina uzima wa milele x2

  1. Maisha yangu nakutolea, uzima wangu nakupa wewe, njoo kwangu Yesu wangu (nimekupa moyo wangu na mwili wangu ukae kwangu) x2

  2. Chakula changu ni mwili wako, kinywaji changu ni damu yako, nishibishe siku zote, (meza yako ya thamani nitajongea unishibishe) x2

  3. Mapenzi yako yamenigusa, maneno yako ni taa Yangu, niongoze maishani, (nakuita Yesu wangu Karibu kwangu uishi nami) x2

  4. Ee Mungu Baba, Mwana na Roho, ewe Utatu Mtakatifu; munitie nguvu mimi,(munijaze roho yangu na neema tele, neema ya Mbingu) x2

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page