Ninakuabudu Ee Mungu Wangu
- Anonymous
- Nov 18, 2023
- 1 min read
Ninakuabudu e Mungu wangu
Japo wafichika ninakutazama
Nakuona kwa imani ee Mungu wangu
Chini ya maumbo hayo ya hostia
Ninakuabudu Mungu kwa moyo
Na kunyenyekea kwa moyo wote
Namwamini Yesu Mwana wa Mungu
Chini ya maumbo hayo ya hostia
Alipofuka Yesu juu ya msalaba
Wabaya wakasema eti kashindwa
Na hata watu wema wamemfuata
Umungu wake wala hautashindwa
Mafahamu yangu yasidanganywe
Yanapo kuona na kukuguza
Yesu Mungu Mwana na Mungu wa kweli
Chini ya maumbo hayo ya hostia
Ee Yesu mfichika sasa nakuona
Hili jambo moja naomba sana
Utakapo fufuka nikuone kwa uso
Nipate heri ya utukufu wako

Comments