Ninakulilia Bwana
- Hymsco Library

- Nov 3, 2023
- 1 min read
Bwana uwe nami katika taabu zangu, kimbilio na ngome yangu ni wewe Mungu wangu. (Ninakulilia Bwana mchana na usiku ee Bwana Mungu wangu unisikilize x2.
Toka vilindini nimekulilia Bwana usikie sauti yangu Bwana: Bwana sikia dua zangu
Bwana kama ungehesabu maovu, nani angesimama mbele yako: Bwana kwako kuna msamaha
Bwana amejaa huruma na neema, Bwana haoni hasira upesi, Bwana Mungu ni mwingi wa fadhili
Nimemngoja Bwana roho yangu imengoja neno lake nimetumaini na roho yangu inamshangilia Bwana

Comments