top of page

Ninapeleka Neno

  1. Ninapeleka bibilia yangu, ni neno jema kutoka kwa Baba

Tulitangaze, (neno), neno la Mungu (Baba), neno la wokovu, laleta uzima x2.

  1. Mapadriwote simameni shangwe, watawa wote tukuzeni neno.

  2. Vijana wote sifuni muumba, wazee wote hii ni siku yenu.

  3. Wakina mama imbeni kwa shangwe, wakina baba chezeni kwa shangwe.

  4. Wadudu wanarukaruka shangwe, wakisikia neno lake Bwana.

  5. Wanyama wanachezacheza shangwe, wakisikia neno lake Bwana.

  6. Neno la Mungu linapenya sana, ni neno jema neno la baraka.

  7. Chezeni ngoma chezeni kayamba, tuimbe kwa furaha alelluya.

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page