top of page

Niongoze Vyema

  1. Nahangaika hapa duniani, maisha yangu hayana furaha Najua wazi hapa si nyumbani, bali njia ya kupita Niongoze vyema Maria, maria Mwema, Bondeni huku niliko nifike kwa usalama Mbinguni kwa Yesu mwanao

  2. Vita na shari vyote vyanisonga, mashaka mengi yaniingia Mwili a roho havina kinga hatari imezidia

  3. Mama Maria ndiwe jibu langu hapa safarini unisaidie Unipombee kwa mwanao Yesu anikinge anilinde

  4. Kwa kuwa Yesu ni Mwokozi wangu nakusihi Mama Nakusihi sana uzifikishe kwake shida zangu anionee huruma

  5. Kumbuka Mama, Yesu alisema, Mama yangu Mwema Tazama mwanao, nawe Yohana huyu ndiye mama yako

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page