top of page

Nisamehe Bwana

Updated: Dec 25, 2023


  1. Nisamehe Bwana mimi mtumishi wako, naja mbele yako naja na sala yangu, ninanyenyekea chini ya miguu yako, unitakase kwa makosa yangu yote

  2. Sistahili mimi kuikaribia meza, wala hata kunena jambo lolote, nimejuta sana naomba huruma yako, unipokee mimi mtumishi wako

  3. Ninapokuomba Bwana unisikilize, mahangaiko ya dunia mengi sana, yamenisonga kushoto hata kulia, mbele mbele na nyuma mimi sioni kitu

  4. Ndugu zangu nao wananichekelea, ninapopambana na hali hali zangu, hivyo tumaini langu naliweka kwako, njoo hima Bwana wangu uniokoe

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating

Recent Posts

bottom of page