Nitajongea Meza
- Anonymous
- Oct 31, 2023
- 1 min read
Nitajongea meza yako Bwana Yesu Mwana wa Mungu unishibishe x2.
Wewe ni mkate, wa uwinguni unishibishe.
Wewe ni maji, ni ya uzima, niburudishe.
Wewe mzabibu, nami ni tawi, nisitawishe.
Wewe msamaha, kwa watu wote nihurumie.
Wewe msaada, wa wasafiri nisaidie.
Wewe ni njia, ya uwinguni uniongoze.
Nazo furaha, za uwinguni ukanijaze.
Niishi nawe, ee Yesu wangu milele yote

Comments