Nitamtolea Bwana Sadaka
- Anonymous
- Oct 30, 2023
- 1 min read
1. Umenilinda siku zote Bwana Mwokozi, nami Bwana nakurudishia shukrani hivi leo.
Sadaka, sadaka nitamtolea Bwana Mungu wangu,Sadaka ilio safi kwa moyo wangu wote daima x2
2. Sadaka yangu japo ni kidogo ee Bwana, nakuomba uipokee na kisha unibariki.
3. Nimevutiwa na huruma yako tukufu, nami Bwana takutolea sadaka hii milele.
4. Moyoni mwangu hakika sijui ee Bwana, walakini kwa wema wako Bwana umeniponya.

Comments